Monday, November 19, 2012

BONGO KAMA ULAYA SASA PICHA ZA X


WABONGO NA PICHA ZA X


Na Mwandishi Wetu

Warembo wa Tanzania waliojitambulisha kwa jina moja moja la Amina, Janie na Candy wamepiga picha za utupu (x) na kuzisambaza sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.

Gazeti hili lilifanikiwa kupata picha za baadhi ya warembo hao hivi karibuni wakiwa katika mitindo mbalimbali ya mahaba. Aidha nyuma ya picha hizo warembo hao wameweka namba zao za simu za mikononi pamoja na mitandao wanayopatikana.

Kufuatia kuwepo kwa mawasiliano ya mabinti hao, gazeti hili liliamua kuwapigia kwa nyakati tofauti na kufanikiwa kumpata Janie aliyedai yupo Arusha kikazi. Janie alisema kuwa, angerudi jijini baada ya siku tatu na kama kuna mtu anahitaji huduma yake aweke mihadi naye kwa sababu alikuwa na ‘oda’ nyingi jijini Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine gazeti hili liliamua kufungua mitandao iliyoainishwa katika picha hizo na kukuta mambo ya kusikitisha. Katika mitandao hiyo warembo hao wameweka bei za huduma wanazozitoa na pindi mteja anapokubaliana nazo humtumia picha mbalimbali za utupu ili kumshawishi.

Hata hivyo, warembo hao wanaodaiwa kushiriki mashindano ya urembo jijini Dar es Salaam katika ngazi ya vitongoji, wameambatanisha ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya Kiingereza kuwa hawatoi huduma ya siku nzima. “Do you need a body to rest? Just call 07..45..*6 for short time only, no room for full time,” unasomeka ujumbe huo.
Gazeti hili limeshindwa kuchapisha namba na mitandao wanayopatikana warembo hao kwa sababu maalum.

No comments:

Post a Comment